Jeshi la Israel, IDF limepeleka divisheni yake ya 36 Gaza City, ambayo ni ya tatu, kama sehemu ya mashambulizi yake ya ardhini dhidi ya wanamgambo wa Hamas.
Awali divisheni hiyo inayojulikana pia kama Ga’ash ilifanya operesheni kusini mwa Gaza ikiwemo Khan Younis, kabla ya kuondoka.
Israel imesema mashambulizi hayo yanalenga kuisambaratisha miundombinu ya kijeshi ya Hamas na kuhakikisha usalama kwa raia wa Israel.
Vitengo vilivyo chini ya divisheni ya 162 na 98 tayari vinaendesha operesheni Gaza City, huku vikizidi kusonga mbele zaidi katika mji huo.
Mashambulizi hayo yanafanyika wakati ambapo jumuia ya kimataifa inaonya kuhusu raia kushambuliwa, huku mashirika ya kutoa misaada yakielezea kuongezeka kwa vifo vya raia na uhaba mkubwa wa chakula, maji na vifaa vya matibabu.
