Kamandi ya Kusini ya Jeshi la Marekani (SOUTHCOM) ilidai kuwa meli hiyo, Sagitta, ilikuwa imekiuka marufuku iliyowekwa na Rais Donald Trump.

Kupitia mtandao wa X, kamandi hiyo ilisema: “Marekani imejitolea kuhakikisha kuwa mafuta pekee yanayoondoka Venezuela ni yale yanayopitia njia halali za kisheria.”

Utekaji huo ni sehemu ya operesheni za wiki za hivi karibuni, baada ya Trump kutangaza kile alichokiita “marufuku kamili ya meli zote za mafuta kuingia na kutoka Venezuela”.

Trump analishutumu taifa hilo la Amerika Kusini kwa kuiba mafuta, ardhi na mali nyengine za Marekani na amesema lazima mali hizo zirejeshwe.

Mnamo Januari 3, Jeshi la Marekani lilimpinduwa na kumteka nyara rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro na sasa linamshitaki kwenye mahakama ya New York kwa madai ya madawa ya kulevya.