Jeshi la Urusi limedai kukikamata kijiji kingine kwenye jimbo la Dnipropetrovsk na kuzidi kuingia kwenye maeneo ya Ukraine, huku hatua za kupatikana kwa makubaliano ya amani kwa mara nyingine zikikwama.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imeesema vikosi vyake vimeteka eneo la Zaporizke, ambako hivi karibuni wanajeshi wa Urusi waliingia kwa mara ya kwanza tangu vita vilipozuka miaka mitatu na nusu iliyopita.
Urusi imeanzisha mashambulizi ya droni ya usiku kucha nchini Ukraine, ikilenga mkoa wa mpakani wa Sumy na kumuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine tisa, hii ikiwa ni kulingana na Gavana Oleh Hryhorov mapema leo, kupitia mtandao wa Telegram.
