Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa amewataka wananchi kujiunga na vifurushi vya Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya wakati taratibu za utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote zikikamilika.

Ametoa wito huo leo katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Mkoa wa Singida Kitaifa.

“Mmegusia suala la bima ya afya na hapa nataka niseme sheria ya Bima ya Afya kwa Wote Sura namba 161 ilitungwa na kuanza kutekelezwa Mwezi Agosti Mwaka jana 2024 kwa baadhi ya vifungu, ili kuwezesha utekelezaji wa sheria hii kikamilifu, serikali inaendelea kushirikisha wadau na makundi mbalimbali ya wananchi, kufanya utambuzi wa Kaya zisizo na uwezo kuboresha mifumo ya utoaji wa huduma na kuandaa vitita vya mafao hivyo kwa wakati huu ninawasihi wastaafu katika sekta binafsi kujiunga na bima ya afya kupitia vifurushi vinavyotolewa na NHIF wakati tukisubiri taarifa za utoaji wa Bima ya AfyakwaWote,” amesema Mhe. Rais.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa