Jeshi  la Kujenga Taifa (JKT), linawaita vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2025 kutoka shule zote za Tanzania bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2025.

Hayo yamesemwa leo Mei 27, 2025  na Kaimu Mkuu wa Utawala wa  JKT, Kanali Juma Mrai, amesema kuwa pamoja na wito huo, JKT limewapangia makambi watakao kwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia Mei 28 hadi  Juni  8,2025.

Kanali Mrai amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha vijana kujengewa uzalendo, umoja wa kitaifa, kufundishwa stadi za kazi na maisha pamoja na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa.

Kanali Mrai amesema vijana hao wamepangwa katika kambi tofauti ikiwemo kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Mpwapwa, Makutupora JKT – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Makuyuni – Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma, JKT Itaka – Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa – Rukwa, JKT Nachingwea – Lindi, JKT Kibiti- Pwani pamoja na Oljoro JKT- Arusha.

Aidha Kanali Mrai amesema kuwa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho wanapaswa kuripoti katika kambi ya Ruvu JKT Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

“Orodha kamili ya majina ya vijana hao,Makambi ya JKT waliopangiwa na maeneo makambi hayo yalipo na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo,inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.mil.tz“

ORODHA YA WANAFUNZI HII HAPA https://www.jkt.go.tz/