Na Kulwa Karedia, Jamhuri Media-Kigoma
Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Taifa imeleeza sababu za mgombea urais wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan kushinda uchaguzi mkuu ujao.

Imesema sababu kubwa ni maendeleo makubwa yanayoonekana maeneo mbalimbali.
Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Katosho mkoani Kigoma leo Septemba 14, 2025.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Fadhil Maganya amesema kwa mara ya kwanza katika historia, wananchi wa vijijini hawalazimiki tena kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za afya na elimu kutokana na miundombinu ya majengo na upatikanaji wa dawa.

Amesema maendeleo hayo ni matokeo ya uongozi wa kisasa wenye dira, uthubutu na maono ya mbali.
Amewataka wananchi wa Kigoma kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, kuichagua CCM pamoja na wagombea wake wote.



