Na Mwandishi Wetu, Singida
MWANASIASA kijana na Mtaalam wa masuala ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba cde Japhari Saidi achukua fomu ya kuomba kuteuliwa na CCM kugombea Ubunge Singida Mjini.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu cde Japhari ameeleza kuwa kilichomsukuma kuchukua fomu ni dhamira yake ya dhati ya kutoa nguvu na jasho lake kuwatumikia kama ambavyo wao walitoa nguvu na jasho lao kumlea na kumsomesha.
“Mimi ni matunda ya nguvu na jasho walilotoa wananchi wa Singida Mjini katika kujenga shule ya Utemini na Dr. Salmini ambapo mimi nilipata bahati ya kusoma, kulelewa na kujengewe misingi ya maadili na uongozi. Sina cha kuwalipa zaidi ya kurejea nami kutoa nguvu na jasho langu kuwatumikia” Alisema
Japhari ni Mkaguzi Mwandamizi wa Dawa katika Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).



