Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia Dar es Salaam

TANZANIA ni kati ya nchi ambayo imebarikiwa kwa kuwa na utajiri mkubwa si wa mali pekee pia umetokana na jinsi Watanzania walivyo ukilinganisha na nchi nyingine.

Hayo yamebainishwa na David Kafulila mbaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia nchini (PPPC), wakati akizungumza majadiliano kuhusiana na masuala ya mwenendo wa uchumi wa nchi.

Kafulila alisema kuwa utajiri wa Tanzania hautokani na uwingi wa maliasili kama madini, mito, maziwa, milima, ardhi yenye rutuba bali ikiwemo pia tabia za watu wake.

“Hivyo tabia ambayo wanayo Watanzania tayari ni utajiri kwani wengine hawapo hivyo kwani Watanzania ni waungwana na wastarabu na jinsi sisi tulivyo hivyo tabia hiyo tu ni uwekezaji tosha” alisema.

Alisema kuwa kuna maendeleo mengi yamefanyika kwa muda mrefu na bado miradi mingi ya kimaendeleo inatekelezwa na haya kwa hatua hiyo Tanzania imeendelea kukua kimaendeleo ukilinganisha mwaka kwa mwaka.Kuna mambo makubwa yamefanyika na haya nazungumza si kwa sababu ya kuwa kuna uchaguzi.

“Tumeanza kutekeleza Dira ya miaka 25, chini ya Serikali ya Awamu ya Sita ambayo inakwenda kutekeleza Dira ya mwaka 2050 ni dira ya miaka 25 ijayo kwani si kipindi kirefu sana katika mipango ya maendeleo.

“Dira hii tunapaswa kujadili zaidi,tunaweza kujadili kwa mapana zaidi. Pia hatuwezi kukwepa msingi wa Serikali mwaka 2026/27 wakati Dira itaanza kutekelezwa kwani ndiyo inashikiliwa kwa uchumi” alisema.

Alisema kuwa Tanzania inaweza ikawa na Dola trilioni 1 katika kipindi cha miaka 25 ambapo ukitazama nchi ambazo zimetimiza dola ya trilioni 1 zipo 19 tu ambazo zipo kwenye klabu ya trilioni 1 katika nchi zote duniani 193.

“Ukiangalia nchi hizo zenye dola trilioni 1, Tanzania kuna kazi kubwa ipo mbele yetu ili tufike, ukiangalia sekta ya umeme nchi ndogo inazalisha megawati zaidi ni 53 unaweza kuangalia ni jukumu gani ambalo lipo mbele yetu.

“Kutoka hapa kwenda huko, nchi ambayo ilifanikiwa kujenga uchumi kwa dola trilioni 1 kwenda mbele miaka 23 na 25 ilikuwa na uchumi kama wetu na ikafanikiwa kujiunga ni Korea Kusini , walifanya nini hadi kufika huko lakini pia inaonyesha kuwa inawezakana lakini inahitaji mabadiliko ya kila kitu ikiwemo hata sisi wenyewe kubadilika.

“Ikiwa inahitaji mabadiliko unatakiwa kubadilika kwendana na mahitaji hayo au kutoka ili kusudi akae mtu anayeweza kwendana na mahitaji hayo na usipobadilika utabadilishwa” alisema Kafulila.

Aliongeza kuwa wakati Rais Samia akizindua Dira 2050 pale Dodoma, aliitaka Serikali kuangalia upya mifumo ya kitaasisi, kisheria, kisera ili kuhakikisha kuwa tunafikia hayo matarajio yetu ya kwenye Dita 2050.

“Nimegusa kidogo kuhusu dira na namna ya kutoa mchango jinsi ya kufika huko kwani wote tuna wajibu kuhakikisha kuwa tunafika huko matarajio yetu na kiasi gani kufikri na namna ya kutoa mchango kuliko hata kulaumiana kwa sababu wote tuna wajibu wa kujenga nchi kwa namna yoyote kwa viwango vyovyote kwa nafasi yako inayoyesha pia inawezakana” alisema.

TATHMINI YA MWENENDO WA UCHUMI

“Tukitathmini mwenendo wetu kwa miaka hii minne kwa kiasi ni tumejenga msingi , nimejaribu kutazama awamu zote za Serikali kwa maoni yangu mimi ni kuwa katika kipindi miaka hii minne katika uchambuzi watu wanaotoa maoni kwa awamu jinsi ya kujenga hiyo dira , maoni yake ni kuwa nchi kwa awamu zote ya kwanza 1, 2, 3, 4, 5,na hata hi ya 6 mambo makubwa yanayoamua maendoeleo ya uchumi ni manne.

“Nimeangalia mwenendo wa uchumi kwa ujumla wake na ukizungusha na nimesoma kwa Mwinyi, Mkapa, Jakaya, Magufuli na sasa namsoma Rais Samia kwa nchi zote unaamua mwelekeo wa uchumi wake kwa jambo la kwanza ambalo nchi zote duniaani inaangalia ni ubora wa rasilimali watu ‘Human capital’.

“Hili ni jambo la kwanza ambalo katika mwenendo wa uchumi linatazwa kwani ni msingi katika ukuaji wa uchumi hapa unaweza kuwafundisha watu ujasirimali na kuwafanya watu kuwa akili ya kijasirimali.

“Hii imekuwa hivyo kwa awamu kwanza na kuwafundisha watu wawe na akili ya ujasirimali, baada tukasafiri huko, bada siku ya mazishi ya baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere alipofika Rais wa Benki ya Dunia moja ya kitu ambacho alikioa katika miaka 1960 ni suala ‘human capital’ ambayo leo ni ajenda kubwa duniani.Ubora wa rasilimali watu ni moja ya kitu ambacho inaweza kuamua” alisema.

Anaongeza kuwa katika utafiti uliofanywa na Oxford 2014 walionyesha kwamba mataifa makubwa tajiri 13, makubwa duniani ni asilimia 62 utajiri ulitokana na ubora watu na maliasili ni asilimia inachangia asilimia 5 tu wa utajiri wake, ufanisi wa kitaasisi ni asilimia 25.

“Sio kwamba hawana maliasili hapana, China wanazalisha dhahabu nyingi sana kuliko nchi yoyote duniani lakini dhahabu sio mjadala kwao lakini kuna vitu vya ziada vya teknolojia ukizungumza teknolojia unazungumza ubora wa watu zao la ‘human capital’.

“Tumepambana kutoka Serikali ya Awamu ya 1, 2,3, 4, 5, na sasa ni 6 kwenye kujenga ubora wa rasilimali watu kwenye kujenga ubora wa rasilimali watu” alisema.

Kafulila alisema kuwa ukiangalia Serikali ya Awamu ya Sita ni kitu gani ambacho tunaweza kukiona ukiachilia mbali katika miaka minne cha kwanza ni ongezeko la bajeti kutoka sh trilioni 4 hadi sh trilioni 6 ni ongezeko kubwa .

“Mbali ya mabadiliko makubwa ya kutoka elimu bure, elimu bila ada, kutoka awamu ya tano hadi ya sita, ukiachilia mbali mabadiliko ya mitaala kwenye ‘transfomation’ ya elimu, awamu ya sita imefanya makubwa kuhakikisha kuwa inatatua changamoto kwa jamii si kwani dunia inabadilika kwa kasi sana.

“Mabadiliko ya bajeti, mitaala kwenye sekta ya elimu ni uwekezaji mkubwa elimu ya juu na elimu ya kati ili kujenga usawa kwenye elimu. Uamuzi wa kutoa elimu mikopo kwenye elimu ya kati ni eneo moja zaidi imefanya makubwa zaidi kwa kuzidi kuongeza ubora , kurekebisha masuala ya bumu ambapo awali walikuwa wakipata sh 8000 na sasa ni sh 10,000.Bado zaidi tunatakiwa kufanya ni kwenda zaidi ambako wenzetu wamefika” alisema.

Uwekezaji sekta ya afya wa Serikali ya Awamu wa ya Sita sekta ya afya ni mkubwa sana kwenye uwezekaji watalii imeongezeka ukilinganisha na huko nyuma, kliniki za watoto zimejenga 114 kwa kipindi cha miaka minne, vituo kwa ajili ya huduma za dharura zilikuwa 7 sasa zipo 125 ni mafanikio makubwa kwa kipindi kifupi sana. “kwenye ‘economy equestion’ unasema mzungunko ni miaka saba lakini hii ipo kwa mzunguko wa miaka minne haya yanapaswa kufanyika zaidi katika ukifikiri katika kipindi cha miaka 25 ijayo.

Vifo vya akinana mama wajazito na watoto chini ya miaka mitano vimepungua ingawawa changamoto zipo lakini ubora umeimarika na ubora zaidi ni gharama zaidi na imeokoa vipaji ambavyo zilikuwa zikipotea.

Anasema kubwa changamoto tuliyonayo ni kuwepo kwa ongezeko kubwa la watu kuliko ongezeko la wastani la watu dunia na kuliko ongezeko la watu Afrika ambapo asilimia 3 kwa mwaka ongezeko ongeko la watu dunia ni asilimia 1, Afrika ni asilimia 2.

“Ni wajibu kwa kila familia kujisimamia na kuwa na idadi ya familia unayoweza kuisimamia na yenye lishe bora kuhakikisha tunawezekeza zaidi kwenye eneo hilo kuanzia eneo la kaya kwani kubwa kwenye afya lishe bora.

“Hadi kwenye maji watu wanazungumza unaweza kupima afya, lishe wataalamu wanashauri kuhakikisha kuwekeza zaidi eneo hilo ni kipengele kikubwa kwenye maarifa ni afya hata hivyo kwenye zaidi kwenye miradi ya maji kwani inaokoa dola 4 ambazo zingetumika kutibu magonjwa yanayotokana na magonjwa ya maji safi na salama” alisema.

Aliongeza kuwa mkakati wa serikali Awamu ya Sita uwekezaji kwenye huduma ya maji ni kubwa sana mimi nimekaa bungeni, hakuna utekekezaji wa maji mkubwa kama huu uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita mefikia upatikanaji amaji ni asilimi 83 ni hatua kubwa.

‘Serikali imedhamiria kufanya mapinduzi makubwa kwenye huduma maji, kilimo na sisi tuna kazi ya kufanya katika kuhakikisha kuwa miradi hii inasimamiwa kikamilifu.