Na John Walter, JamhuriMedia, Arusha

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Angela Kairuki ametoa miezi mitatu kwa taasisi mbali mbali ambazo zinahusika na Uchakataji,Ukusanyaji na Usambazaji wa taarifa binafsi kukamilisha usajili wake mara moja.

Kairuki amesema kuwa Sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi ni wezeshi ambayo imeweka misingi muhimu nane ya kuzingatia,ukusanyaji uchakataji na usambazaji taarifa ndani na nje mipaka Tanzania, hivyo amesema kuwa mafunzo hayo yakawe chachu ya kurekebisha mifumo ya utendaji wa kazi.

Kairuki ameyasema hayo Jijini Arusha wakati kufunga mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi yaliyofanyika katika kituo Cha kimataifa(AICC), Arusha.

Kairuki amesema kuwa serikali kwa kutambua kuwa Tanzania sio kisiwa iliamua kutunga Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi mwaka 2023,ikiwa ni pamoja na majukum mengine ilitoa elekezo la uanzishwaji wa tume ya ulinzi wa taarifa binafsi (PDPC).

“Tunaamini mtakuwa mabalozi wazuri katika utekelezaji wa Sheria hii haswa ukizingatia Arusha ni Jiji la Utalii lenye huduma nyingi ambazo zinahusisha ukusanyaji wa taarifa binafsi tunaamini hatatuangusha kila Afisa awajibike kuzingatia kanuni za uhalali,uwazi,madhumuni mahsusi,Usalama wa taarifa na heshima ya faragha ya wadau na wateja wake”Alisisitiza Waziri Kairuki

Amesema kuwa kama serikali haitakubali uzembe,visingizio katika matakwa ya Sheria kwa kuwa muda wa kujisajili uliotolewa na serikali umekwisha.

“Mheshimiwa Raisi dkt.Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 03,April 2024,Alitoa maelekezo kwa kuanza utekelezaji wa kusajili kwa hiari taasisi zote,na alielekeza ifikapo tarehe 31,Desemba,2024 utekelezaji uwe umeanza wa usajili wa taasisi na Maafisa wa ulinzi wa taarifa binafsi lakini baadaye Tume yetu pia ikatoa nyongeza ya muda kutoka tarehe 31 Desemba 2024,mpaka tarehe 31 April 2025,Leo hii hapa ni 2026 utaona ni zaidi ya mwaka”Alisema Kairuki

Aidha amesema kuwa hakutakuwa na huruma tena kwa kuwa muda uliotolewa ulitosha kujisajili na ifikapo April 08,2026 hatua zitachukuliwa kwa taasisi ambayo itakaidi Agizo hilo la mheshimiwa Raisi.

Mwenyekiti wa bodi wa Tume hiyo bw.Adadi Mohamed amesema kuwa tume itaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wajue wajibu kwa kuwa uchumi wa kidigitali unaendana na Utalii.

Amesema kuwa kutotekeleza Sheria ya ulinzia wa taarifa binafsi ni kuweka rehani faragha, Usalama na haki za misingi za wahusika ambao ni wananchi wanaohudumiwa na katika taasisi hizo.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Dkt. Emmanuel Mkilia amesema kuwa mafunzo hayo yalilenga kuandaa Maafisa rasilimali watu wenye uwezo wa kusimamia wa kusimamia ulinzi wa taarifa binafsi ndani ya taasisi za Umma na binafsi.

Dkt.Mkilia amesema kuwa kusudio lake ni kuhakikisha kuwa ukusanyaji, uchakataji,uhifadhi na matumizi ya taarifa binafsi yanafanyika kwa kuzingatia kikamilifu matakwa ya Sheria kanuni na viwango vya kitaaluma vinavyolinda haki ya faragha na wananchi kwa mujibu wa Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi.

Jumla ya taasisi zilizipatiwa mafunzo hayo ni 178,28 kutoka taasisi za serikali,38 taasisi za Utalii na 112 kutoka taasisi nyinginezo.