Kardinali Robert Prevost, mmisionari Mmarekani ambaye alitumia maisha yake nchini Peru na ambaye anaongoza ofisi yenye ushawishi mkubwa ya maaskofu katika Vatican, amechaguliwa kuwa Papa wa kwanza Mmarekani katika historia ya miaka 2,000 ya Kanisa Katoliki.


Prevost, mwenye umri wa miaka 69, amechukua jina la Leo wa XIV.

Moshi mweupe ulitoka kwenye bomba la moshi la Kanisa la Sistine leo saa 12:07 jioni kwa saa za huko, kuashiria kwamba kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki amechaguliwa.