Na Mwandishi Wetu, Jamhuri Media, Zanzibar

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Taifa, Mohamed Ali Kawaida amesema mgombea urais wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Hussein Mwinyi walitumia vizuri fedha za Covid kwa kujenga hospitali, barabara na hospitali.


Kawaida ametoa kauli hiyo, leo Septemba 17,2025 alipopewa nafasi ya kusalimia maelfu ya wafuasi wa chama hicho Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa chama hicho.


Amesema wamekubaliana vijana wote Oktoba 29, mwaka huu, watatoka na kwenda kuwachagua viongozi wote kwa maana ya Rais Samia na Dk Ali Hussein Mwinyi na wabunge, wawakilishi na madiwani wote wa chama hicho.