Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo Omar Said amesema kwamba ACT Wazendo haikubaliani na maamuzi ya kutenguliwa kwa mgombea urais Luahaga Mpina kwa kile walichodai kuwa yamefanywa kinyume na Sheria na Katiba.

“Tume Huru ya Uchaguzi(INEC) haina mamlaka kisheria kumuengua mgombea yoyote wa nafasi yoyote kwa kufuata maelekezi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ama taasisi youote ,badala yake mtu au taasisi inaruhusiwa kuweka mapingamizi kwa mgombea inayemtilia shaka,”amesema.

Aidha,amesema kwamba nakala ya Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliyotumwa Tume Huru ya UchaguI haijaonesha sehemu yoyote ambayo Msajili wa Vyama vya Siasa inaiomba Tume Huru ya Uchaguzi kumtengua mgombea  wao, hivyo kuendelea kuhoji uharaka wa INEC kuchukua maamuzi.

“Tumeamua kukimbilia mahakamani kwa sababu Mahakama ndio chombo cha mwisho chakutoa haki hapa nchini,hivyo ni imani yao hoja zao zitapokelewa ma kukubalika “,amesema.

Advocate John Seka ni wakili wa anaeongoza jopo la mawakili upende wa ACT Wazalendo na Vivian Method ana ongoza jopo la mawakili wa Tume Huru ya Uchaguzi.