Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia
Dodoma
Serikali imepanga kuongeza kiwango cha chini cha pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu wanaolipwa moja kwa moja kutoka Hazina kwa karibu asilimia 150, kwa mujibu wa bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26 iliyowasilishwa leo.
Akiwasilisha bajeti bungeni Juni 12, 2025, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema hatua hiyo inaonesha jinsi Serikali ya Awamu ya Sita inavyotambua mchango mkubwa wa wastaafu katika maendeleo ya taifa.
“Katika kutambua huduma yao kwa taifa, serikali itaongeza pensheni ya chini ya kila mwezi kwa wastaafu wanaolipwa kupitia Hazina kutoka Shilingi 100,125.90 hadi Shilingi 250,125.90, sawa na ongezeko la asilimia 149.8. Mabadiliko haya yataanza kutekelezwa kuanzia Julai 2025,” Dkt. Nchemba.
