Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kikiendelea usiku huu Jijini Dodoma tarehe 28 Julai, 2025 kupitia na kuchuja mapendekezo ya majina ya wagombea wa Ubunge wa Majimbo, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Viti Maalum vya Ubunge na Baraza la Wawakilishi.