Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) (Panel of Elders, POE) akiwa katika picha ya pamoja na Profesa Arthur Peter Mutharika, Rais wa Malawi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya SADC, baada ya kufanya naye mazungumzo jana Ijumaa jijini Lilongwe, Malawi.

Pamoja nao ni Mama Joyce Banda, Rais Mstaafu wa Malawi, ambaye ni Mjumbe wa Jopo hilo la Wazee. Katika mazungumzo yao, pamoja na mambo mengine, Viongozi hao walipata fursa ya kumweleza Rais Mutharika kuhusu kazi zilizofanywa na zinazoeandelea kufanywa na POE katika kusuluhisha migogoro katika nchi za Ufalme wa Lesotho, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi na kwa sasa Madagascar.

Kimuundo, POE ni moja ya vyombo vya kuzuia migogoro na kurejesha amani katika nchi za SADC ambacho kinaripoti moja kwa moja kwenye Asasi ya SADC Troika, ambayo nchi ya Malawi ndiyo Mwenyekiti wake kwa sasa.