Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameapa kuendelea kuiunga mkono Urusi katika maeneo yote ikiwa ni pamoja na katika vita vyake nchini Ukraine.
Vyombo vya habari vya Serikali ya Pyongyang vimesema mapema leo kwamba Kim Jong Un alipokutana na afisa wa ngazi za juu wa usalama wa Urusi Sergei Shoigu siku ya Jumatano, alisema Pyongyang “itaunga mkono bila masharti msimamo wa Urusi na sera zake za kigeni katika masuala yote muhimu ya kisiasa na ya kimataifa likiwemo la Ukraine.
Pande hizo mbili aisha zimekubaliana kuimarisha zaidi uhusiano.
Urusi na Korea Kaskazini zilitia saini makubaliano mapana ya kijeshi mwaka jana, ikiwa ni pamoja na kifungu cha ulinzi wa pande zote, wakati wa ziara ya nadra ya Rais wa Urusi Vladimir Putin nchini humo.
