Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema hana sababu ya kuyakwepa mazungumzo na Marekani kama nchi hiyo haitomshinikiza kuachana na silaha za Nyuklia.
Akizungumza katika hotuba yake mbele ya bunge Jumapili 21.09.2025, Kim alisisitiza kuwa kamwe hatoachana na silaha hizo ili nchi yake indolewe vikwazo.
Kauli ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini imetolewa wakati serikali ya Korea Kusini ikitoa wito kwa Rais wa Marekani Donald Trump azungumze na Kim miaka sita baada ya mazungumzo yote ya amani kuvunjika. Majadiliano ya kipindi cha nyuma na serikali ya Pyongyang yalisitishwa kutokana na vikwazo na kutakiwa iachane na silaha za nyuklia.
