Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Maswa
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Maisha Mtipa kwa kutimiza maelekezo ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kutenga fedha ya asilimia 10.
Hayo amezungumza jana wakati akipokua kwenye makabidhiano ya mwenge huo kutoka Wilaya ya Maswa chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Vicent Anney na Mkuu wa Wilaya ya Meatu Fauzia Ngatumbura.
Ussi amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa Maisha amefanya kazi KUBWA sana ya kuhahakikisha anatimiza maelezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani ili kuweza kuwafikia, wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.

” Kipekee kabisa nikupongeze sana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hii ya Maswa kaka yangu Mtipa kwa kuhakikisha unapokea maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kutumia mapato ya ndani ya asilimia 10 na kurudisha kwa wanajamii” huku ni kumuunga mkono juhudi za Mh. Rais hongera sana Kwa kazi nzuri Mkurugenzi.
Aidha Ussi amefafanua kuwa Halmashaurihiyo chini ya Mkurugenzi…pia imetoka sehemu ya mapato yake na kurudisha kwa jamii Kwa kuchangia jumla ya sh.mil. mil.112 katika shughuli za miradi ya Maendele, huku wananchi nao wakiwa wamechangia jumla ya sh.mil.5 katika shughuli mbalimbali za miradi ya Maendeleo inayopitiwa na Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025.
” Mkurugenzi wa Maswa huyu, yeye pamoja na timu yote wameendelea kutimiza wajibu wao kwa sababu wameendelea kumuunga mkono Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa anazoendelea nazo za kuwaletea Maendeleo Wanzanzania wote Kwa kufikiwa na asilimia 10 na kurudisha mapato yake ya ndani Kwa wananchi ” amesema Ussi.

Pia Ussi amempongeza Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt Vicent Anney pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama kwa kuhakikisha Maswa bado inaendelea kuwa salama na kuwajibika katika kuhamasisha wananchi kujiletea Maendeleo ya wilaya yao Kwa kufanya kazi kikamilifu na si vinginevyo.
” Mkuu wa Wilaya na Kamati Yako mmefanya kazi nzuri sana Toka Jana hadi Leo mnapoukabidhi mwenge wa Uhuru wilaya ya Meatu, miradi mizuri yote tumeliona , ambayo itakwenda kuonyesha sura nzuri ya wilaya ya Maswa, hongera sana Mkuu wa Wilaya.
” Na niwapongeze sana Wana Maswa, kwa sababu miradi ambayo tumeitembelea imegusa karibia kila sekta , tumegusa sekta ya miundombinu ya afya, tumegusa miundombinu Elimu, tumegusa miundombinu ya Maji, tumeenda kugusa miundombinu Barabara, lakini pia tumejionea miradi mkubwa na mizuri ndani ya wilaya hii ya Maswa, itakayoweza kuonyesha alama nzuri katika jamii na kumpa heshima kubwa Mh.Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan” ameongeza Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi .

Hata hivyo Ussi ameongeza kuwa Mwenge wa Uhuru umeendelea kudumisha upendo, haki, umoja na mshikamano kwa jamii kwa kufanya shughuli mbalimbali na kubwa za Maendeleo katika nchi ya Tanzania.
