Upepo wa kasi umepita, vibes kama loote linasikika, nyomi la watu limefurika yoote ni katika mapokezi makubwa ya Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 aliyewasili na kupokelewa na Maelfu ya wananchi wa Ussa River wilayani Meru mkoani Arusha, leo tarehe 1 Oktoba 2025.
Dkt. Samia yumo mkoani Arusha kwaajili ya kunadi ilani ya uchaguzi ya CCM (2025/30) , Sera na Ahadi zake katika kuelekea miaka 5 ijayo pamoja na kuomba kura kwa wananchi hao.
Huu ni muendelezo wa mikutano ya kampeni za Urais na sasa ni zamu ya Mkoa wa Arusha.
