Klabu ya Simba SC imepoteza kwa bao 1–0 dhidi ya Petro Atletico de Luanda katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa leo, Novemba 23, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 78 na kiungo Benardo Oliveira Dias, maarufu kama “Benny”, akiipatia Petro Atletico ushindi muhimu ugenini.
Kwa matokeo haya, Simba wanalazimika kusaka ushindi katika michezo yao ijayo ili kuongeza matumaini ya kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.


