Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia
Dar es salaam
Kikundi Cha mama lishe Kawe”Ngome ya mama” Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na kampuni ya Camgas -Camel Oil Ltd,kimeamdaa kongamano la kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia litakalofanyika Msasani Beach Agost, 26 Mwaka huu.
Kongamano hilo litahusiana na utoaji wa Elimu ya Matumizi sahihi ya gesi safi kupikia ili jamii iweze kuachana na matumizi ya Nishati chafu ikiwemo kuni na mkaa ambayo imekua ikiathiri afya pamoja Mazingira.

Hayo amesema Agosti 21,2025 na Mratibu Mkuu wa Kongamano hilo Potipoti Ndanga amesema kuwa kufanyika kwa kongamano hilo ni kutokana na utafiti walioufanya kuanzia ngazi ya Serikali ya mtaa,huku kaulimbiu yake ikiwa ni”Gesi safi ni habari ya Mjini”.
” Nawaomba wakazi wa Wilaya ya Kinondoni kupitia jimbo la Kawe, na kata zake zote 20,tumefanya utafiti kuanzia ngazi ya chini(grassroots) kwa wenye viti wa Serikali za mtaa na tukapata mpishi bora mmoja kwenye kata ambaye atakwenda kuwakilisha kata katika Mashindano ya kumpata mpishi bora kwenye kongamano hilo.
“Tumewapata akina mama na kutoka kata 20,ambao watakuja kwenye Mashindano ambayo Jimbo la Kawe ni kata 10 na Kinondoni ni kata 10.

Naye Mtendaji wa Kata ya Kawe Husna Nondo amesema kuwa kutumia Nishati safi ya kupikia inasaidia kuweka Mazingira Safi katika Manispaa hiyo.
“Tunataka kata zetu zote 20 za Manispaa ya Kinondoni,ikiwemo kata ya Kawe Mitaa,na wafanyabiashara waweze kutumia Nishati safi ya know,na siku ya kongamano tutatoa Elimu mbalimbali juu ya matumizi bora ya Nishati Safi kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan”
Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya Camgas-Camel Oil Ltd ambao ni wadhamini wa Kongamano hilo Sadiq Abrt amesema kuwa yeye kama mwekezaji Mzawa ameamua kuwa mdhamini Mkuu wa Kongamano hilo ikiwa ni kuunga mkono Serikali katika jitihada za kutangaza matumizi ya Nishati safi ya kupikia.

Aidha Ndanga amesema kuwa lengo ni kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekua kinara katika kutangaza Nishati Safi ya kupikia,sasa kama Rais wa Nchi anatumia Gesi safi ya kupikia,kwanini wewe Mwananchi tunaenda wapi,tunafanya nini tusitumie gesi safi ya kupikia?
“Sisi CamGas tunatambua jitihada za Serikali hivyo siku ya Kongamano tutatoa punguzo kwa Wananchi watakao nunua majiko ya gesi ili kuhakikisha jamii inatumia Nishati hii muhimu ambayo hai athiri afya na Mazingira ya Wananchi” amesema.

Kwa upande wake Balozi wa Kampuni hiyo Dotto Magari amewahamasisha wananchi kuachana na matumizi ya Nishati Chafu na badala yake watumie Nishati safi ikiwemo Gas ya kupikia itokanayo na Kampuni ya Camgas.
“Kwa kuanzia kongamano hili tutalizindua kwa mara ya kwanza katika Wilaya ya Kinondoni maeneo ya Msasani Beach siku ya terehe 26 mwezi huu,lakini tunampamgo wa kufanya kongamano hili Mkoa wote wa Dar se salaam,na tutakua na Mashindano ya kutafuta mshindi bora wa upishi ambaye atapatiwa zawadi ya jiko la gas” amesema Janguo.