Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Bagamoyo

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametembelea kiwanda cha kuunganisha magari aina ya FAW cha Rostar Vehicle Equipment Ltd ,wilayani Bagamoyo na ameridhishwa na kazi kubwa inayoendelea kufanyika .

Amepongeza wawekezaji hao kushirikisha vijana wa Kitanzania kupata ajira na mafunzo ya kuunganisha magari hayo.

“Vijana wana uwezo! Ni wabunifu, wachapakazi na wenye ,” alisema Kunenge . “

Mkurugenzi wa kiwanda, Bai Xinguo, alieleza ,kiwanda hicho cha kuunganisha magari ya FAW ni kikubwa Barani Afrika.

“Kiwanda hiki kinatarajia kuunganisha hadi magari 500,000 kwa mwaka na tayari kimepokea oda ya magari 1,000 kutoka kwa wateja mbalimbali. Pia kitaproduce trailers, matanki (tanks) na cranes.”

Hata hivyo, aliomba Serikali kusaidia kuboresha barabara ya kufika kiwandani ambapo mkuu wa mkoa alhaj Kunenge aliahidi kushughulikia suala hilo kwa kushirikiana na mamlaka husika.

Vilevile Kunenge alimuagiza ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo kuanza upangaji wa mji na kuhakikisha wamiliki wa ardhi wanafuata ramani ya mipangomiji.