
Maboresho ya miundombinu yaliyochangia ongezeko la Shehena ambapo kwa kipindi cha miezi kumi na moja kwa mwaka 204/2025 mizigo imeongezeka kwa asilimia 11, ambapo imehudumia tani mil 23.9 kulinganisha na tani mil 21.5 za miezi 11 ya mwaka 23/24.
Uwekezaji uliofanywa na DP World pamoja na TEAGTL umepelekea ongezeko la shehena mchanganyiko kutoka tani milioni 15.29 sawa na ongezeko la asilimia 11 ukilinganisha na kipindi ambacho TPA ilikuwa ikiendesha magati hayo kwa mwaka 2023/24 (tani milioni 13.75).
Hali kadhalika, ongezeko la shehena limeonekana pia kwa upande wa makasha ambayo yameongezeka kutoka makasha ya futi ishirini (TEUs) 1,159,387 sawa na ongezeko la asilimia 28 ikilinganishwa na makasha (TEUs) 904,424 yaliyohudumiwa katika kipindi kama hiki mwaka uliopita
(2023/24).
DP World ameshawekeza bilioni 214 Bln na kabla ya June ataongeza bilioni 100, huku kampuni ya TEAGTL imeanza uwekezaji wa bilioni 410.
Kupungua kwa Muda wa Meli Kusubiri Nangani, muda wa meli kuhudumiwa bandarini (ship turnaround time) unaojumuisha muda wa kusubiri nangani umepungua katika Bandari ya Dar es Salaam kutoka wastani wa siku 30 (mwaka 2023/24) hadi kufikia wastani wa siku 6 mwaka 2024/25 kwa meli za makasha. Kwa sasa, meli za makasha zinazohudumiwa na DP World hazisubiri nangani na uhudumiwa moja kwa moja gatini pindi zinapowasili kwa muda wa wastani wa siku 4.
Gharama za uendeshaji kwa upande wa TPA hususan katika Bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa wastani wa asilimia 40 kufuatia ushirikishaji wa DP World na TEAGTL katika utekelezaji na uendeshaji wa shughuli za bandari.
Hali hii imeimarisha uwiano wa faida kwa TPA kutoka wastani wa
asilimi 4 (Shilingi za Tanzania Bilioni 49) kwa mwaka 2023/24 hadi kufikia wastani wa asilimi 36 (Shilingi za Tanzania Bilioni 329) kwa mwaka 2024/25.
Manufaa mtambuka, katika kipindi kinachoanzia mwezi Septemba 2024 hadi sasa, kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha zaidi ya miaka mitatu (3),
Bandari ya Dar es Salaam imeweza kuhudumia shehena mbalimbali
zinazosafirishwa na wafanyabiashara kwa ajili ya biashara za mwisho wa
mwaka bila ya kuwepo kwa malalamiko ya kucheleweshwa kwa shehena hizo kutoka kwenye meli ambazo zilikuwa zikisuburi kwa muda mrefu sana nangani ukilinganisha na kipindi kama hiki mwaka 2023.

