Licha ya mashabiki wa Simba kupata furaha ya mpira, lakini tamasha la leo pia lilikuwa na burudani mbalimbali za wasanii tofauti, ambao waliwapa raha mashabiki .

Tamasha la Simba Day 2025 lilihitimishwa kwa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati Wekundu wa Msimbazi Simba SC dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Mchezo huo wa kirafiki umefanyika Septemba 10, 2025 ambapo Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia mchezo ambao umehitimisha sherehe za Simba Day 2025 uliopigwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Mbao ya Simba SC yamefungwa na Abdulrazak Hamza dakika ya sita ya mchezo na Steven Desse Mukwala dakika ya 65 na kufanikuwa kupata ushindi katika mchezo huo muhimu.

Katika mchezo huo Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso, amemwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, kama Mgeni Rasmi katika kilele cha Wiki ya Simba.