Dkt. Phillip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amekabidhi tuzo kwa Wizara ya Uchukuzi na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kwa kutambua kazi nzuri iliyofanywa katika huduma za udhibiti usafiri ardhini kwa kuzingatia vigezo vya utawala bora, uboreshaji utoaji huduma, matumizi ya mifumo, kiwango cha kuridhika kwa wateja na ongezeko la wateja ambapo LATRA imeibuka Mshindi wa Pili miongoni mwa taasisi za Serikali zinazotoa huduma na zisizofanya biashara.


Tuzo hizo zimetolewa tarehe 24 Agosti 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa – Arusha (AICC) ikiwa ni sehemu ya kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoratibiwa na ofisi ya Msajili wa Hazina ambapo Prof. Godius W. Kahyarara Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi alipokea tuzo ya Wizara ya Uchukuzi na Prof. Ahmed M. Ame Mwenyekati wa Bodi ya LATRA akiambatana na CPA Habibu J. Suluo Mkurugenzi Mkuu LATRA walipokea tuzo ya LATRA.