Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Dar es Salaam
Kituo cha Sheria na Haki za binadamu kimehuisha kwa kusaini Mkataba Mpya wa makubaliano wa miaka 3, kuanzia 2025-2027 na Ubalozi wa Norway kupatiwa Ufadhili wa fedha kiasi Dola Milioni mbili zitakazosaidia katika Mpango kazi mkakati 2025-2030 katika kusaidia wananchi ikiwemo Msaada wa kisheria,kutoa Elimu usawa wa kijinsia na kuendeleza kazi za kutetea haki na demokrasia kwa Watanzania.
Akizungumza Septemba 8,2025 Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Fulgence Massawe katika hafla ya utiaji saini huo mesema Kituo hiko kumekuwa na mahusiano ya muda na Ubalozi wa Norway tangu 2013 na kimeshaipatia Ufadhili Milioni 61.

” Norway itaendelea kuwa Mfadhili wetu Mkuu fedha hii wanazozitoa ni kusaidia Kituo katika shughulia mbalimbali ikiwemo mashauri kwa Umma,masuala ya kijinsia,Msaada wa kisheria,mashauri ya kimkakati ” amesema Massawe
Naye Balozi wa Norway nchini, Bi. Tone Tinnes, amesema “Makubaliano haya yanaonyesha dhamira yetu ya muda mrefu na Norway katika kusaidia wananchi na Kwa kuunga mkono LHRC, tunachangia jamii yenye haki za kisiasa, maridhiano, uwezeshaji wa wanawake na uhuru wa kujieleza, ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.”

“Haki za kisiasa na maridhiano ni msingi wa imani na utulivu. Demokrasia imara inategemea uhuru wa kujieleza na sauti huru, na Norway inajivunia kuunga mkono kazi za LHRC kulinda utu na thamani ya binadam”amesema Balozi
Aidha Kupitia msaada huo, LHRC itaendelea kushughulikia mageuzi ya kisheria, masuala ya uchaguzi, haki za wanawake na watoto, pamoja na kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi.

