Na Tatu Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Dalaam
Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu tayari amepandishwa kizimbani leo Juni 2, 2025 kwaajili ya kusubiri kutajwa kwa kesi mbili za jinai zinazomkabili ikiwemo uhaini na kuchapisha taarifa za uongo.
Lissu ameingia mahakamani hapo kusikiliza mojawapo ya kesi zinazomkabili ikiwemo ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni ambapo Mahakama inaanza kupokea ushahidi wa Serikali
Wanachama wa CHADEMA pamoja na viongozi mbalimbali wa Chadema akiwemo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, Godbless Lema, Katibu Mkuu wa zamani wa chama hicho, Dkt Wilbroad Slaa wamejitokeza Mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo.

