Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha ACT Wazalendo umefanya uamuzi mkubwa kwa kumchagua rasmi Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kupitia tiketi ya chama hicho.

Katika zoezi la upigaji kura lililohusisha wajumbe 610, wajumbe wote walipiga kura ambapo kura halali zilikuwa 605 na kura tano (5) zilikataliwa au kuharibika Mpina alipata jumla ya kura 559, akimshinda mpinzani wake Aaron Kalikawe aliyepata kura 46.

Aidha, chama hicho kimemtangaza Bi. Fatma Abdulhabib Ferej kuwa mgombea mwenza wa urais, akiungana na Mpina katika kinyang’anyiro hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.

Uteuzi huu unaweka msingi wa kampeni za ACT Wazalendo kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025, chama hicho kikiwa na matarajio makubwa ya kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini.