Mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamechukua sura mpya baada ya waasi wa M23 kuishutumu serikali kwa kutumia mamluki wa kigeni kushambulia maeneo wanayoyadhibiti, ikiwemo eneo la makazi la Kadasomwa, lenye migodi katika wilaya ya Kalehe, mkoa wa Kivu Kusini.

Msemaji wa M23, Lawrence Kanyuka, amesema mashambulizi hayo ya anga kupitia ndege zisizo na rubani yamesababisha vifo vya raia na maelfu kutawanywa wakikimbia mashambulizi hayo. 

Serikali ya Kongo mjini Kinshasa haijathibitisha rasmi kuhusu kutumia mamluki, lakini madai ya M23 yameibua hisia kali kutokana na kumbukumbu za Januari, pale mamia ya mamluki Romania walipojisalimisha baada ya waasi hao kutwaa mji wa Goma na kuruhusiwa kurejea kwao kupitia Rwanda. Kanyuka ameonya kuwa safari hii hatima yao haitakuwa kama ile ya awali. CHANZO DW