Makadinali 133 kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamejumuika mjini Vatican kushiriki zoezi muhimu na la kihistoria la kumchagua papa atakayemrithi hayati Papa Francis aliyeongoza Kanisa Katoliki kwa miaka 12.
Mjumuiko huu maarufu kama conclave umeanza shughuli hiyo katika kanisa dogola Sistine ambapo makadinali watabaki hadi pale papa mpya atakapochaguliwa.
Mjumuiko wa makadinali ni muhimu sana kwa waumini bilioni 14 wa Kikatoliki kote duniani. Makadinali hao ambao wote wako chini ya umri wa miaka 80 wametokea mabara matano wanatarajiwa kumchagua kiongozi ambaye atakuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazoibuka katika dhehebu hilo zama hizi.
Miongoni mwa hizi ni mgawanyiko ndani ya kanisa, kushuka kwa kiwango na mahudhurio kanisani na kutatua madai ya kashfa za ngono.

