Madaktari bingwa nchini China wamefanikiwa kwa mara ya kwanza kufanya upandikizaji wa mapafu kutoka kwa nguruwe hadi kwa binadamu. Wanasema hilo linaoyesha uwezekano wa mafanikio katika utaratibu huo.
Wanasema hilo linaoyesha uwezekano wa mafanikio katika upasuaji huo hata kama majaribio makubwa zaidi bado yanahitajika. Kwa mujibu wa Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya njia ya hewa ya mji wa Guangzhou, mapafu hayo aliyowekewa mtu ambaye ubongo wake umepoteza uwezo wa kufanya kazi yalimsaidia kupumua na kuipa damu hewa ya Oksijeni kwa muda wa siku 9 bila matatizo.
Wanasayansi wanasema utafiti huo unanuwia kukabiliana na uhaba wa viungo muhimu vinavyohitajika kote duniani kwa matibabu.
Hata hivyo, mapafu yanakuwa na ‘changamoto tofauti za kipekee’ kutokana na ‘uchangamano wake wa anatomia na kifiziolojia au ufanyaji kazi wa viungo vya viumbe.’
Miongoni mwa mambo mengine, muingiliano wa moja kwa moja wa mapafu na hewa ya nje kwa kawaida huongeza hatari ya maambukizi.
