๐ถ Sekta yaongezeka kwa kasi, yajenga miundombinu na kuinua wananchi
Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Morogoro
Mauzo ya madini ya dhahabu mkoani Morogoro yamefikia Shilingi bilioni 16.51 katika kipindi cha Julai 2023 hadi Septemba 2025, yakionesha kasi kubwa ya ukuaji wa sekta ya madini na mchango wake katika uchumi wa mkoa.
Mapato ya Serikali kupitia sekta hiyo pia yameendelea kupanda kutoka Shilingi bilioni 2.67 mwaka 2021/2022 hadi Shilingi bilioni 4.9 mwaka 2023/2024, huku Morogoro ikitarajia kukusanya Shilingi bilioni 6.5 katika mwaka wa fedha 2025/2026.

Ofisi ya Madini ya Mkoa wa Morogoro inasimamia shughuli za madini katika wilaya za Gairo, Kilosa, Mvomero na Morogoro.
Akizungumza katika mahojiano maalum, hivi karibuni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Zabibu Napacho, alisema kuwa mkoa huo umebarikiwa na aina nyingi za madini ikiwemo Feldspar, Rhodolite Amethyst, Green Garnet, Dhahabu, Kaolin, Shaba, Ruby, Spinel, Marble, Graphite, REE na Quartz.
Alifafanua kuwa jumla ya leseni za uchimbaji mdogo zilizotolewa ni 2,413, za uchimbaji wa kati 205, wakati leseni za uchimbaji mkubwa ni 10 na leseni za utafiti mkubwa zikiwa 61, hatua inayolenga kuimarisha shughuli za madini na kuvutia uwekezaji zaidi mkoani humo.

Kwa upande wa sekta binafsi, Meneja wa Mgodi wa Yusra A. Yusuph, Isack Mushi, alisema mgodi huo unazalisha Dolomitic Marble kwa ajili ya kutengeneza tiles, rangi na bidhaa nyingine, sambamba na kuchangia maendeleo ya jamii.
Alibainisha kuwa mgodi huo umejenga ofisi ya kijiji yenye thamani ya Shilingi milioni 28, umenunua kiwanja cha ofisi kwa Shilingi milioni 4, umeunganisha umeme, kuboresha barabara, kuchimba kisima pamoja na kutoa ajira 65.
Naye Mkurugenzi wa Mangiolin Gems Limited, Shamaina Bashir, alisema kuwa kampuni yake imejikita katika biashara ya vito na uongezaji thamani, huku ikitoa ajira kwa wanawake na vijana ili kuwawezesha kujitegemea na kurejea shule kupitia akaunti za malengo.

โTangu kuanza Julai 2024, vijana 10 wamerudi shule na wengine 10 wapo katika maandalizi ya kujiendeleza mwakani,โ alisema.
Bashir alisisitiza kuwa dhamira ya kampuni hiyo ni kuifanya sekta ya madini Morogoro kuwa chanzo thabiti cha mapato na kichocheo cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.




