Maelfu ya watu wamejitokeza katika mitaa ya mji mkuu wa Denmark wa Copenhagen hivi leo, kupinga azma ya Rais Donald Trump ya kutaka kuichukua.
Maelfu ya watu wamejitokeza katika mitaa ya mji mkuu wa Denmark wa Copenhagen hivi leo, kupinga azma ya Rais Donald Trump ya kutaka kuichukua Greenland inayojitawala na pia ikiwa sehemu ya Denmark. Maandamano hayo yanafuatia onyo la Trump alilolitoa siku ya ijumaa kwamba anaweza kuanzisha ushuru kwa nchi zinazopinga mipango yake ya kulidhibiti eneo la Greenland lenye utajiri mkubwa wa madini.
Maandamano hayo pia yamegongana na ujio wa ujumbe wa wabunge wa Marekani kutoka pande zote mbili za kisiasa, ambao umeweka wazi kuwa Wamarekani wengi wanapinga vitisho vya kijeshi vinavyotolewa na utawala wa Trump.
Moja ya chama cha watu wa Greenland wanaoishi Denmark cha Uagut, kilisema lengo la maandamano hayo ni kutuma ujumbe wa wazi na wa pamoja wa kuheshimu demokrasia ya Greenland na haki za msingi za binadamu.

