Mwishoni mwa wiki ya Siku ya Wapendanao, Bolt Tanzania ilishuhudia ongezeko la mahitaji ya safari katika jiji la Dar es Salaam, huku maeneo ya Masaki, Oysterbay, Mbezi Beach na Leader’s Club yakionesha kuwa ni vituo vilivyotumika zaidi kushushia na kusafirisha abiria.
Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji yanayokua kwa kasi barani Afrika, likikadiriwa kuwa na wakazi takriban milioni 9 mwaka 2026 — ongezeko kubwa kutoka milioni 5.38 waliokadiriwa katika Sensa ya Taifa ya mwaka 2022.
Takwimu za kitaifa pia zinaonesha kuwa idadi ya vijana nchini ni kubwa, ambapo takribani asilimia 77 ya Watanzania wako chini ya umri wa miaka 35 — kundi linalochangia kwa kiasi kikubwa mahitaji ya huduma za usafiri kwa ajili ya chakula cha jioni, matembezi na burudani kupitia Bolt.
Eneo la Slipway pekee lilirekodi zaidi ya safari 1,000 zilizoelekezwa huko. Aidha, Carlos Bastos maarufu kama Kalito, mwanzilishi wa mgahawa wa Wavuvi Kempu, aliwahamasisha wafuasi wake zaidi ya 198,000 kwenye Instagram kutumia Bolt, akieleza kuwa maegesho ya mgahawa huo yalikuwa yametumika kwa tukio maalum la Valentine.
“Mfumo wa usafiri unaochochewa na teknolojia unaimarisha maisha ya kijamii na kiuchumi ya jiji. Kila safari kuelekea mgahawani, ufukweni au kwenye maeneo ya burudani inaunga mkono sio tu watoa huduma bali pia mtandao mpana wa wafanyabiashara wadogo.
Hata wauza maua wadogo wa St. Peters hutumia Bolt Send kuwasilisha maua kwa wapendwa wao katika kipindi hiki. Kwa vijana wengi, usafiri si suala la kufika tu — ni sehemu ya safari ya kujenga mahusiano binafsi na kitaaluma,” alisema Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Afrika Mashariki.
Kwa madereva wa Bolt, msimu kama huu wa Valentine hauleti tu shughuli nyingi bali pia fursa za kuongeza kipato. Ongezeko la safari limewawezesha kuongeza mapato na kushiriki mafanikio hayo na familia na wapendwa wao. Hii inaonesha namna majukwaa ya usafiri yanavyoshiriki kikamilifu katika kuchochea uchumi na maisha ya kijamii ya Dar es Salaam.
Kadiri Dar es Salaam inavyoendelea kukua, ndivyo pia umuhimu wa usafiri salama na wa kuaminika unavyozidi kuwa sehemu ya namna wananchi wanavyofanya kazi, kuunganishwa na kusherehekea matukio muhimu ya maisha — safari moja baada ya nyingine.



