JamhuriComments Off on Makamu wa Rais amuaga Jenista Mhagama
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameshiriki katika Ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Joakim Mhagama, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska, Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma. Tarehe 13 Desemba 2025. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Joakim Mhagama, mara baada ya kuaga mwili huo iliyofanyika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska, Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma. Tarehe 13 Desemba 2025.