Makamu wa Rais awasili Uganda – kushiriki mkutano wa Jumuiya ya Maziwa Makuu
JamhuriComments Off on Makamu wa Rais awasili Uganda – kushiriki mkutano wa Jumuiya ya Maziwa Makuu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe nchini Uganda leo tarehe 20 Desemba 2025. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu, utakaofanyika tarehe 21 Desemba 2025.