Na Mwandishi Wetu, Jamhuri Media, Arusha
Mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Paul Makonda (CCM),amesema kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan imeacha matokeo chanya.
Makonda ametoa kauli hiyo alipopewa nafasi ya kusamilia wananchi wa mkoa wa Arusha wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia leo Oktoba 2,2025.

Amesema kazi kubwa zilizofanywa na Rais Samia ndani ya mkoa wa Arusha zilizoacha alama na matokeo chanya kila kona ya Arusha, ni kipimo tosha cha wananchi kukichagua chama chake.
Amesema kazi ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Arusha ambao ambapo amesema hivi sasa zipo ndege ndogo utoka Arusha kwenda Nairobi nchini Kenya muda wote.
Amesema hiyo ni dalili njema ya kuendelea kufungua mkoa wa huo sasa uwanja huu unapokea ndege kutoka nje ya nchi moja kwa moja tofauti na awali ilivyokuwa wakilazimika kwenda viwanja vingine kupata vibali.
“Upanuzi wa uwanja huo ni fursa kwa wafayabiashara na watalii kutoka nje ya nchi kupunguza gharama na kupoteza muda mwingi,”amesema.
Amesema kupitia maelekezo ya Rais Samia, mkoa huo umefanikiwa kutekeleza miradi iliyokwama kwa miaka mingi ambapo zaidi ya Sh bilioni 64 zimetumika.

Amesema katika jimbo la Arusha Mjini tayari ujenzi wa stendi kubwa na ya kisasa umeanza kujengwa pamoja na soko kubwa la kisasa pia linajengwa.
Amesema wananchi wa mkoa huo, wanafurahia uongozi bora wa serikali ya awamu ya sita inayotokana na CCM kwakuwa kulikuwa na changamoto ya umeme lakini sasa ufumbuzi umepatikana.
“Uamuzi huu jambo zuri limezidi kupania wigo wa upendo wa Watanzania wote kwa CCM,”amesema.

Katika hatua nyingine, Makonda amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kumuamini na kuamini katika vijana.
“Na𝘬𝘶𝘴𝘩𝘶𝘬𝘶𝘳𝘶 𝘬𝘸𝘢 𝘯𝘺𝘢𝘬𝘢𝘵𝘪 𝘻𝘰𝘵𝘦 𝘬𝘶𝘯𝘪𝘢𝘮𝘪𝘯𝘪 𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘯𝘪𝘱𝘢 𝘩𝘦𝘴𝘩𝘪𝘮𝘢 𝘬𝘸𝘢 𝘯𝘢𝘧𝘢𝘴𝘪 𝘻𝘢 𝘶𝘵𝘶𝘮𝘪𝘴𝘩𝘪 𝘬𝘢𝘮𝘢 𝘔𝘸𝘦𝘯𝘦𝘻𝘪 𝘸𝘢 𝘊𝘊𝘔, 𝘮𝘬𝘶𝘶 𝘸𝘢 𝘮𝘬𝘰𝘢 𝘸𝘢 𝘈𝘳𝘶𝘴𝘩𝘢 𝘯𝘢 𝘩𝘢𝘵𝘪𝘮𝘢𝘺𝘦 𝘬𝘶𝘱𝘪𝘵𝘪𝘢 𝘷𝘪𝘬𝘢𝘰 𝘷𝘪𝘬𝘶𝘣𝘸𝘢 𝘷𝘺𝘢 𝘤𝘩𝘢𝘮𝘢 𝘬𝘶𝘯𝘪𝘳𝘦𝘫𝘦𝘴𝘩𝘢 𝘯𝘢 𝘣𝘢𝘢𝘥𝘢𝘺𝘦 𝘬𝘶𝘴𝘩𝘪𝘯𝘥𝘢 𝘬𝘶𝘳𝘢 𝘻𝘢 𝘮𝘢𝘰𝘯𝘪 𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘳𝘦𝘫𝘦𝘴𝘩𝘸𝘢 𝘵𝘦𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘨𝘰𝘮𝘣𝘦𝘢 𝘶𝘣𝘶𝘯𝘨𝘦 𝘬𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢 𝘫𝘪𝘮𝘣𝘰 𝘭𝘢 𝘮𝘫𝘪𝘯𝘪..”
” Mwenyekiti 𝘚𝘢𝘮𝘪𝘢 𝘸𝘦𝘸𝘦 𝘯𝘪 m𝘢𝘮𝘢 𝘮𝘸𝘦𝘮𝘢 𝘴𝘢n𝘢, 𝘶𝘮𝘦𝘴𝘪𝘮𝘢𝘮𝘪𝘢 𝘷𝘪𝘬𝘢𝘰 𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘯𝘪𝘵𝘦𝘶𝘢 𝘬𝘸𝘦𝘯𝘺𝘦 𝘯𝘢𝘧𝘢𝘴𝘪 𝘮𝘣𝘢𝘭𝘪𝘮𝘣𝘢𝘭𝘪, 𝘣𝘢𝘥𝘰 𝘶𝘮𝘦𝘦𝘯𝘥𝘦𝘭𝘦𝘢 𝘬𝘶𝘵𝘶𝘭𝘦𝘢 𝘷𝘪𝘫𝘢𝘯𝘢, 𝘔𝘶𝘯𝘨𝘶 𝘸𝘢 𝘮𝘣𝘪𝘯𝘨𝘶𝘯𝘪 𝘢𝘬𝘶𝘵𝘶𝘯𝘻𝘦 𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘬𝘶𝘭𝘪𝘯𝘥𝘢..”amesema.


