Mwanamke wa Afrika Kusini aliyepatikana na hatia ya kumteka nyara na kumsafirisha bintiye mwenye umri wa miaka sita amehukumiwa kifungo cha maisha jela pamoja na wenzake wake wawili.

Racquel ‘Kelly’ Smith (35), mpenzi wake Jacquen Appollis na rafiki yao Steveno van Rhyn wanadaiwa kumtorosha binti huyo kwa ahadi ya kulipewa randi 20,000 ($1,100; £850).

Licha ya kufanyika kwa juhudi kubwa ya kumtafuta msichana huyo uliotangazwa, ambaye alitoweka Februari 2024, hadi sasa bado hajapatikana.

Katika kesi hiyo iliyoendeshwa kwa wiki sita huko Afrika Kusini, baada ya mashahidi kutoa ushahidi na mahakama kuridhika pasipo mashaka Jaji Nathan Erasmus alisema, “Kwa shtaka la kusafirisha binadamu unahukumiwa kifungo cha maisha jela, kwa shtaka la utekaji nyara unahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela,” alisema hakimu huku akishangiliwa na wananchi waliofikamahakamani kusikiliza hukumu hiyo.

Smith, na washirika wake hawakuonyesha hisia zozote wakati hukumu katika kituo cha jamii huko Saldanha ambapo kesi ilifanyika ili kuwaruhusu wakazi wa eneo hilo kuhudhuria kesi.

Hisia zilikuwa juu kabla ya hukumu hiyo, huku wananchi wenye hasira wakisema washtakiwa hao wanapaswa kupata hukumu kali kwa sababu wanastahili.

Kabla ya hukumu, Nyanya yake Joshlin, Amanda Smith-Daniels, alimsihi binti yake amrudishe mjukuu wake au aeleze yuko wapi.

Wakati wa kesi hiyo, mahakama ilisikiliza ushahidi kutoka kwa mashahidi zaidi ya 30, ambao walieleza picha ya maisha ya shida ya msichana huyo na kutoweka baadaye.

Kelly Smith na washirika wake walikataa kutoa ushahidi au kuita mashahidi wowote kwa ajili ya utetezi wao.

Lakini shahidi ambaye alikuwa ni rafiki wa mwanamke huyo Lourentia Lombaard, alisema kuwa mtuhumiwa ni jirani yake ambaye aligeuka kuwa shahidi wa serikali, aliieleza mahakama kuwa jirani yake ambaye ni Kelly Smith alimweleza kuwa amefanya ‘kitu cha kijinga’ na kumuuza mtoto wake Joshlin kwa mganga wa kienyeji, anayejulikana nchini Afrika Kusini .

Naye shahidi mwingine ambaye ni mchungaji alitoa ushahidi kwamba mwaka 2023, alimsikia Smith – mama wa watoto watatu akizungumzia kuwauza watoto wake kwa randi 20,000 ($1,100; £850) kila mmoja, ingawa alisema yuko tayari kukubali kiwango cha chini cha $275.

Alidai kuwa wakati akimweleza taarifa hiyo, tayari binti yake alikuwa tayari kwenye meli, ndani ya kontena, na alikuwa njiani kuelekea Afrika Magharibi.