Na Berensi China, JamhuriMedia, Butiama

Mamia ya wananchi wa Kijiji cha Butiama mkoani Mara na maeneo ya jirani ya Mkoa wa Mwanza, Dar es Salaam na Arusha wamejitokeza katika mazishi ya aliyekuwa mke wa Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamhuri Media Manyerere Jackton marehemu Joyce Simbambili yaliyofanyika katika eneo la Mwitongo kijijini Butiama mkoani Mara.

Akihutubia katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa Manyerere mchungaji Canon Baraka wa Kanisa la Aglikana Dayosisi ya Mara, amesema enzi za uhai wake marehemu Joyce aliishi kwa kutetea imani yake na aliyatoa maisha yake kumtumikia Mungu ambapo aliishi na jamii vizuri ambapo amewataka watoto wake kumuenzi mama yao kwa kufuata yale aliyokuwa akitenda ya kumpendeza Mungu.

“Nawaona baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Jamhuri, marafiki zake Manyerere akiwemo Deodatus Balile na Absalom Kibanda ambao wamepata nafasi ya kumuuelezea marehemu Joyce kwa namna alivyoishi enzi za uhao hivyo watoto mnatakiwa kuiga mfano huo” alisema.

Kaka mkubwa wa familia ya Burito ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere mzee Joseph Butiku amesema marehemu alikuwa nguzo katika familiia yao licha ya kuwa mke lakini pia alikuwa msimamizi wa familia.

Naye Chief Japhet Wanzagi alizungumza kwa niaba ya Serikali amesema msiba huo ni pengo kwa familia ambapo amewataka kumtanguliza Mungu hasa katika kipindi hiki cha maombolezo.

Akitoa Salam za Serikali Mkuu wa Wilaya ya Butiama ,Thecla Mkuchika ameitaka familia hiyo kuwa na moyo wa subira kwani siku zote msiba hauvumiliki hasa unapotokea kwa mtu unayemtegemea.

Mazishi hayo pia yamehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali, siasa, dini, vyama vya kihabari, wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, viongozi kutoka ofisi ya Msajili Hazina, viongozi kutoka taasisi mbalimbali za Serikaki na zisizo za Serikali.

Marehemu Joyce Simbambili tunamuombea apumnzike kwa amani. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe!