Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia,
Dar es Salaam

Culture and Development East Africa (CDEA) kwa kushirikiana na Tamasha, Tuzo za Filamu pamoja Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameandaa maonyesho ya Mashariki Creative Economy Expo 2025 ambapo yatawakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya ubunifu.

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Uzinduzi wa Maonyesho hayo ya Mashariki Creative Economy Expo 2025 au Tamasha na tuzo za filamu itakayofanyika Agosti 14 Hadi 16 Mwaka huu Mlimani City Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Agosti 5,2025 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Culture and Development East Africa( CDEA) Ayeta Wangusa Amesema CDEA kwa kushirikiana na Tamasha na tuzo za Filamu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania imeandaa Maonyesho hayo ya kipekee yatakayokutanisha wajasriamali wabunifu,watunga Sera,wawekezaji na wadau wa Sekta ubunifu kutoka Afrika Mashariki na Maeneo mwingine.

“Maonesho haya yatakuwa ya siku tatu ya Wazi kuanzia saa tatu Asubuhi hadi saa kumi na mbili joini yakihusisha Soko la kazi za ubunifu mitindo,fundi,uchapishaji na Filamu huku mjadala,Mafunzo,na burudani,zote zikifanyika zikilenga kukuza uchumi wa ubunifu jumuishi na endelevu” amesema Ayeta

“Siku ya pili kutakua na mazungumzo kuhusu uchumi wa Muziki, mafunzo ya ubunifu, Muziki, Filamu,mitindo Uandishi, uzinduzi wa ripoti ya UNESCO Afrika Book Industry, kikao cha uwelewa COSOTA na usiku wa shot ambapo utafanyika Nafasi Art Space”

Ameongeza”siku ya mwisho ya maonyesho hayo kutakua na mjadala wa sera za Filamu licha ya kuwa Tanzania hakuna sera tutatumia ya Afrika Mashariki, muendelezo wa mafunzo ya ubunifu, fashion show pamoja vyumba maalum ambapo wafanyabiashara kwenye sekta Filam watakutana na kubadilishana uzoefu na kujifunza mambo mbalimbali kwenye ubunifu.”

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sanaa za Ufundi Basata ,Bona Masenge amesema kwamba wamepokea mradi huo kwa furaha kubwa kwani utakuwa msaada kwa wabunifu kujitangaza kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha ameeleza kwamba kwa sasa kamati maalum ya Kitaifa itakayohusisha wadau mbalimbali imeshaanza vikao ili kuhakikisha taratibu zote zinazohitajia zinakamilika na pia amewataka wadau na wasanii wachangamkie fursa hii kwa kujisajili ili kushiriki maonesho hayo.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Bodi ya Filamu, Emmanuel Ndumukwa amesema kwamba hii ni fursa kwa wasanii kujifunza na kutumia nafasi hiyo kubadilisha uzoefu kutoka kwa wasanii wengi na jinsi ya kutumia mafunzo hayo kutumia nafasi za matumizi sahihi ya motandao ya kijamii ili kujipatia fedha.

Aidha Culture and Development East Africa(CDEA)ni nyumba ya Maarifa na Kituo cha fikra za ubunifu kilichopo Dar es salaam,Tanzania hujishughulisha na kukuza Sekta ya ubunifu kupitia Utafiti,uvumbuzi na majukwaa ya kuwawezesha wasanii na Wajasriamali wa ubunifu kutoka Afrika Mashariki kwa maelezo zaidi tembelea ww.masharikiexpo.com