MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amewahutubia Wananchi kwenye mkutano mdogo wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa CCM,Kata ya Sanya Juu ndani ya jimbo la Siha, Wilayani Siha,akiendelea na mikutano yake ya Kampeni leo Jumamosi Septemba 13,2025 mkoani Kilimanjaro.

Baada ya kuwasalimia Wananchi hao,Dkt Nchimbi ambae ni mgombea mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,pia alitumia nafasi hiyo kuwanadi Wagombea Ubunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Siha Ndugu Godfrey Mollel pamoja Diwani.

Dkt.Nchimbi ambae ameingia Kanda ya Kaskazini,akianzia mikutano yake ya Kampeni Mkoani Arusha na sasa ameingia mkoa wa Kilimanjaro kusaka kura za ushindi wa Kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.

Ngombea mwenza huyo amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.