Rais wa Marekani Donald Trump anasema kuwa Iran “imekubali” masharti ya mkataba wa nyuklia na Marekani.
Trump alielezea mazungumzo ya hivi punde kati ya nchi hizo mbili, ambayo yalimalizika Jumapili, kama “mazungumzo mazito” ya “amani ya muda mrefu”.
Hapo awali, mshauri wa kiongozi mkuu wa Iran aliiambia NBC News kwamba Tehran iko tayari kufanya makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia ili badala yake iondolee vikwazo.
Marekani imesisitiza kuwa Iran lazima isitishe urutubishaji wa madini ya uranium ili kuzuia nchi hiyo kutengeneza silaha za nyuklia – ingawa Iran inasisitiza kuwa shughuli zake za nyuklia ni za amani kabisa.
Akizungumza siku ya Alhamisi nchini Qatar, katika kituo cha pili cha ziara yake ya siku nyingi ya Ghuba, Trump alisema kuwa makubaliano yamekaribia kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na kuongeza kuwa shambulio la kijeshi katika maeneo ya Tehran linaweza kuepukwa.
“Hatutatimua vumbi lolote la nyuklia nchini Iran,” Trump alisema baada ya mkutano huko Doha na viongozi wa biashara.
“Nadhani tunakaribia labda kufanya makubaliano bila kufanya hivi.
“Labda umesoma leo taarifa kuhusu Iran. Ni aina fulani ya kukubaliana na masharti.”
