Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent, ametangaza makubaliano ya ushuru wa forodha kati ya Marekani na China.

Besented: Ushuru kushuka kwa 115%

Bessent amesema baada ya majadiliano “madhubuti”, Marekani na Uchina zimekubaliana kusitisha ushuru uliopandishwa kwa siku 90 “kwa pande zote mbili”, kumaanisha kuwa zote zitapunguza ushuru wao kwa 115%.

China yathibitisha kusimamishwa kwa ‘hatua za kukabiliana na ushuru’ – ripoti

Wizara ya biashara ya China imethibitisha kusimamishwa kwa “hatua zote za ushuru” zilizochukuliwa dhidi ya Marekani tangu Aprili 2, Reuters inaripoti.

Ushuru wa Marekani kwa China ulikuwa 145%

Tunasubiri maelezo zaidi juu ya ushuru mpya – lakini, kama tulivyoripoti, Scott Bessent anasema kila upande utapunguza ushuru wao kwa 115%.

Ushuru wa sasa wa Marekani kwa bidhaa za China ni 145% – wakati China inatoza ushuru wa 125% kwa baadhi za Marekani.

Kwa hivyo habari za leo zinamaanisha kuwa asilimia hiyo inapaswa kushuka hadi 30% na 10% – lakini hilo bado limethibitishwa.