Marekani na Umoja wa Ulaya zimefikia makubaliano ya kibiashara yanayoshusha ushuru kwa bidhaa za Ulaya hadi asilimia 15 kutoka kitisho cha awali cha Rais Donald Trump cha asilimia 30.

Trump na Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen, walitangaza makubaliano hayo nchini Scotland siku ya Jumapili (Julai 27), baada ya mkutano wa saa nzima kati yao.

Trump aliyaita makubaliano hayo kuwa makubwa kabisa kuwahi kufikiwa, akisifia uwekezaji wa Umoja wa Ulayawa dola bilioni 600 ndani ya Marekani na ongezeko kubwa la ununuzi wa nishati vifaa vya kijeshi kutoka Marekani.

Lakini von der Leyen alimuelezea Trump kama mtu mgumu wa kuafikiana naye, na aliwaambia waandishi wa habari kuwa asilimia 15 ndicho kitu pekee walichofanikiwa kukipata.

Ujerumani imesema makubaliano hayo yameinusuru nchi hiyo na hali ngumu ya kiuchumi.