Ukraine imesema Urusi imefanya mashambulizi makubwa ya droni usiku wa kuamkia leo dhidi ya Ukraine na kuua watu 10.
Wengine 38 wamejeruhiwa, majengo kadhaa yakiwemo makaazi ya watu pia yameharibiwa ikiwemo katika mji mkuu Kiev.
Maafisa wa Ukraine wamesema hayo leo huku rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akisema shambulizi hilo lililoua pia mtoto, limeuonyesha ulimwengu, jibu la Urusi kwa juhudi za kidiplomasia za ulimwengu, mnamo wakati rais wa Marekani Donald Trump akijaribu kumaliza vita hivyo.
Katika ukurasa wake wa mtandao wa X, Zelensky amesema Urusi huchagua mashambulizi badala ya mazungumzo. Na kwamba inachagua maafa badala ya kumaliza vita. Ametoa wito wa Urusi kuwekewa vikwazo vipya.
Vikosi vya angani vya Ukraine vimesema vilidungua droni 563 kati ya 598 zilizofyatuliwa na Urusi na vilevile vilizuia makombora 26 kati ya 36 yaliyorushwa na Urusi kulenga maeneo mengi ya Ukraine. CHANZO DW
