Mashambulizi ya anga ya Israel yawaua takriban watu 62, huku mashirika yakionya kuhusu njaa ashambulizi ya anga ya Israel yawaua takriban watu 62, ulinzi wa raia unasema,.
Mashirika mashirika ya kibinadamu pia yanaonya kuhusu njaa kutokana na ukosefu wa chakula
Israel imezidisha mashambulizi yake ya kulipua Gaza huku mazungumzo ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka yakiendelea na Donald Trump yuko safarini Mashariki ya Kati.
Duru za hospitali za eneo hilo zinasema zaidi ya watu 40 wameuawa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya anga ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.
Ripoti zinasema kuwa takriban miili 36 imefikishwa katika hospitali za Khan Younis, kusini mwa Gaza, ambako Israel ilishambulia kwa mabomu makubwa jana usiku.
Wakati huo huo, Israel imewaamuru watu kuondoka katika eneo hilo, jambo ambalo limeongeza hofu zaidi miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.
Haya yanajiri wakati ambapo Israel imekuwa ikizuia misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula na vifaa vya matibabu kufika Gaza tangu mwanzoni mwa mwezi Machi. Jumuiya ya kimataifa imelaani vizuizi hivyo, na Umoja wa Mataifa umeonya kuwa zaidi ya Wapalestina milioni mbili wanaoishi huko wanakabiliwa na “hatari kubwa” ya njaa.
Lakini Israel inakanusha kuwa mtu yeyote huko Gaza anakabiliwa na njaa.
