Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Pemba
Waziri wa Uchukuzi na mgombea ubunge Jimbo la Mkoani, Makame Mbarawa amesema uwanja wa ndege wa Pemba unajengwa na kuwa wa kimataifa.
Mbarawa ametoa kauli hiyo septemba 20, 2025 alipopewa nafasi ya kusamilia maelfu ya wananchi wa pemba wakati wa mkutano wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye uwanja wa Gombani ya Kale.

Amesema utakuwa na urefu kilomita 2.5 na jengo kubwa la kisasa ambalo litakuwa na uwezo wa kubeba abiria 300,000 kwa mwaka na awamu ya pili utabeba abiria 700,00.
Mradi huu utakapokamilika, ndege kubwa aina ya Boing 737 na Airbus 320 ambazo zina uwezo wa kuchukua abiria 160 zitaweza kutua Pemba, maana yake sasa Pemba inakwenda kufunga kwenye sekta ya utalii, na uchumi. Sisi wananchi wa Pemba hatuna cha kukulipa, umefanya kazi kubwa, haijawahi kutokea kuleta miradi hii mikubwa. Gharam ya ujenzi utakuchukua Sh bilioni 500.
Amesema ujenzi wa barabara ya Chake kwenda Mkoani yenye urefu wa kilomita 45 ina changamoto nyingi zikiwamo kona ambazo zinasababisha ajali za mara kwa mara.

Kwa mapenzi makubwa uliyonayo kwa wananchi wa Pemba umeamua barabara hii ijengwe kwa kiwango cha lami, kwenye mji wa Chake na Mkoani kutakuwa na njia nne.Kutoka Chanjaani kuelea boti kutakuwa na barabara nne. Kutakuwa na njia maalumu ya watembea kwa miguu na itawekewa taaa za kisasa. Hatuna cha kukulipa,amesema.
Amesema tayari mkandari yuko uwanja wa ndege na Septemba 25, Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi anakwenda kuanzisha ujenzi wa mradi huo .
Amesema barabara ya Chake-Pemba ilikuwa na kigugumizi, ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 90.
