Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi kumemtaja Mgombea Urais wa ACT Wazalendo , Othman Masoud Othman, atashindwa vibaya katika kinyang’anyiro cha Urais kutokana na uwezo wake kuwa mdogo mbele ya mgombea CCM Rais Dk Hussein Ali Mwinyi .

Pia CCM kimemtaka Othman kujua kuwa upigaji kura kwa siku mbili si suala la kisiasa, hadithi na simulizi bali lipo kwa mujibu wa sheria .

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar , Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo , Khamisi Mbeto Khamis ameeleza hayo huku akimtaka ajiandae kisaikolojia kushindwa vibaya katika Uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.

Mbeto alisema kama yupo mgombea toka upinzani atakayepata matokeo ya kura chache na kuingia katika kurasa za historia ya Chaguzi kuu za Vyama vingi Zanzibar toka Mwaka 1957 hadi 2025 ni Othman.

Alisema atapata matokeo ya aibu kwa kuwa si kiongozi wa kisiasa mwenye historia pia rekeodi ya kutumikia wananchii, badala yake amejiingiza katika siasa kwa kushinikizwa na utashi wa wapambe .

“Othman atashindwa vibaya Urais kwa sababu hayumo katika vitabu vya historia ya siasa za Zanzibar .Ni mgombea dhaifu kuwahi kutokea . Kama si ushabiki , mizengwe na udalali wa wapambe alikataa kugombea Urais ” Alisema Mbeto

Katibu huyo Mwenezi alisema Othman akitaka kujua kama ataanguka vibaya katika Uchaguzi wa mwaka huu,atazame idadi ndogo ya wanachama wa ACT waliojitokeza kumsindikiza kuchukua fomu ya urais .

‘Dalili ya mvua huanza kutanda mawingu .Nyota njema huonekana mapema asubuhi. Kwa hali ya manung’uniko na wanachama kususia ndani ya ACT Othman ataanguka vibaya ifikapo Oktoba “Alieleza

Mbeto alisifu juhudi za utendaji uwezo binafsi ,umakini na utayari wa mgombea wa CCM Dk Mwinyi pamoja na utumishi wake wa miaka mitano iliopita alivyoiletea Zanzibar maendeleo ya haraka.

“Tumejiandaa kisawasawa na sasa tupo tayari kwa kupiga kura .Hatuingii katika uchaguzi huu kwa kubahatisha .Mgombea wetu lazima ashinde” Alisema Katibu huyo Mwenezi.