Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma

MBUNGE wa Viti Maalum, Mwanaisha Ulenge (CCM) ameiomba Serikali kuhakikisha fedha zilizotengwa kufanikisha mradi wa kituo atamizi cha uzalishaji wa bidhaa za mkonge kinachowahusisha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu zinafika kwa wakati kwa walengwa.

Akizunguma bungeni leo Mei 22,2025 bungeni wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo,kwa mwaka wa fedha 2025-2026 Ulenge amesema tayari Serikali imetenga shilingi milioni 600 kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kituo hicho.

“Tunawashukuru sana tunaishukuru Bodi ya Mkonge ya Tanga naomba sana Mheshimiwa Mwenyekiti Wizara ihakikishe milioni 600 zinafika kwa wakati ili tuweze kukuza uchumi wetu,”amesema Mbunge huyo

Mbunge huyo amehimiza bidhaa hizo kuzalishwa kwa wingi ili zitumike ndani ya nchi na pia katika masoko ya kimataifa, hatua itakayosaidia kuongeza thamani ya zao la mkonge na kuinua uchumi wa vikundi vinavyohusika na mradi huo.