Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Babati
Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Manyara Regina Ndege amekabidhi majiko 100 yenye thamani ya sh.mil.5,500,000 Kwa akina mama na baba Lishe wa Kata ya Riroda na Magugu wilayani Babati Mkoani humo ili kuendelea na matumizi ya Nishati safi ya kupikia.
Mbunge Ndege amekabidhi jana majiko hayo kwa walengwa jana mbele ya madiwani wa Viti Maalum wa Tarafa ya Mbugwe Staimili Masasi, Mariam kwimba pamoja na Naomy Richard Sangu.

Ndege amesema kama inavyofahamika kuwa tukio hilo ni katika kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye yuko kwenye kampeni ya kuhakikisha anakwenda kutekeleza kwa asilimia kubwa matumizi sahihi ya Nishati safi ya kupikia.
” Nimekuja Leo kuwaona mama na baba lishe kama inavyofahamika kuwa tukio hilo ni katika kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye yuko kwenye kampeni ya kuhakikisha anakwenda kutekeleza Kwa asilimia kubwa matumizi sahihi ya Nishati safi ya kupikia” amesema Regina Ndege
Aidha amesema anatambua wengi wao mama na baba lishe wamekua wakitumia kuninna mkaa Kwa ajili ya kufanya matumizi ya kupikia hali inaweyoweza kusababisha kutokea kwa madhara mbalimbali kama macho kuwa mekundu kutokana na Moshi unaosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa,mpamoja na majonjwa kama kifua kikuuu ama kansa.
“Najua kabisa kuwa wengi wetu Nishati chafu ya kupikia kwa kutumia kuni na mkaa, vitu ambavyo vina madhara Kwa binadamu,ni kwasababu tu hatuvioni kwa haraka , lakini wapo wanaopata magonjwa ya Kifua kikuu, Kansa, lakini pia wapo akina mama wanaoathirika na macho kuwa mekundu kwasababu ya Moshi unaotokana na matumizi ya Nishati chafu ya kupikia ambayo ni Kuni pamoja na Mkaa” amesisitiza Mbunge Ndege.

Aidha amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye kinara wa matumizi ya Nishati safi ya kupikia Barani Africa nzima kama muasisi lakini ambaye amebeba ajenda kuu ya kuhakikisha Nishati safi ya kupikia inafika Duniani kote.
Naye Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Mbungwe Naomi Richard Sangu amesema anaamini kwamba kupitia wao Mbunge Regina Ndege alijua tu kuwa wapo makundi mengine muhimu wanaohitajika kupatiwa hayo majiko ili kupendana na matumizi sahihi ya Nishati safi ya kupikia.
” Sisi tunaamini ya kwamba kupitia sisi Mh eshimiwa Regina ulijua kabisa tuna uzazi wetu mwingine kwasababu hiyo umewakumbuka mama na baba lishe Leo umewaketea majiko hakika tunakushukuru sana sana, Mwenyezi Mungu akubariki sana, tunakupenda na tunakuombea kwa Mungu unaoendelea na majukumu yako basi Mungu akutunze.

Akizungumza kwa niaba ya akina mama lishe Halima Seleman ameshukuru mbunge Regina Ndege Kwa Kujitoa kwake katika kuwakumbuka na kuwabadilisha kutoka matumizi ya Nishati chafu ya kupikia hadi kuwa katika matumizi sahihi ya Nishati safi ya kupikia.
Hata hivyo akizungumza kwa niaba ya akina baba lishe Swalehe Shilingi ameshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kubuni njia sahihi na yenye tija katika matumizi sahihi ya Nishati safi ya kupikia Barani Africa, ikiwa ni pamoja na kumshukuru Mbunge Regina Ndege Kwa kuwapatia majiko, kitendo ambacho kwao kimeweza kuwatoa katika Nishati chafu huku Sasa wakiwa katika matumizi sahihi ya Nishati safi ya kupikia.
